MV MWANZA HAPA KAZI TU ; YAANZA SAFARI YA KWANZA YA MAJARIBIO YA KIUFUNDI ZIWA VICTORIA

Meli mpya

     Meli Mpya ya kubeba Abiria na Mizigo ya MV Mwanza hapa kazi tu, kwa mara ya kwanza imeanza safari ya kwanza ya majaribio ya kiufundi katika Ziwa Victoria.

     Meli hiyo imeondoka katika Bandari ya Mwanza Kusini ikiwa ni Watu 60, wakiwemo Wahandisi, Wakandarasi na Wataalam waliokuwa wakiijenga.

     Meneja Mradi wa Ujenzi wa Meli ya MV. Mwanza hapa kazi tu Vitus Mapunda amesema majaribio hayo ni ishara ya kukamilika kwa Ujenzi wa Meli hiyo.

     Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya huduma za Meli MSCL  Meja Jenerali Mstaafu John Mbungo amesema Watanzania wanapaswa kuona fahari kubwa ya ushiriki wao katika Ujenzi wa Meli hiyo.

    Wakazi wa Jiji la Mwanza wameipongeza Serikali kwa kukamilisha Ujenzi wa Meli hiyo.

     Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba Abiria 1,200, Tani 400 za Mizigo, Magari Madogo 20 na Malori Matatu unatarajiwa kukamilika Mei 31 Mwaka huu ambapo Ujenzi wake  ulianza Mwaka 2019 ukitekelezwa na Mkandarasi kutoka Korea ya Kusini zikishirikiana na Suma JKT ya Tanzania, Mradi huo umegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 111 za Kitanzania.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.