Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya uimarishaji wa miondombinu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sheikh Abeid Amani Karume.
Mwenyekiti wa Kamati ya usimamizi wa Viwanja vya Ndege, Ndg.Laila Burhan Ngozi amesema hayo wakati wa Ziara maalum ya kukagua miradi ya uimarishaji wa miundombinu katika Uwanja vya Ndege wa Kimataifa wa Amani Abeid Karume.
Amesema utekelezaji wa miradi hiyo unaridhisha kwa Asilimia kubwa licha ya kuwa imeanza kwa muda mfupi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Canal, Abdi Jeni, amesema lengo la Ziara hiyo ni kuangalia miradi mbalimbali ambayo Mamlaka inatekeleza kufuatana na maagizo ya Serikali inayoyatekeleza ikiwemo uimarishaji wa shughuli za anga na uimarishwaji wa Viwanja vya Ndege.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Seif Abdallah Ali, amesema utekelezaji wa miradi unakwenda kuimarisha utoaji wa huduma ndani ya Viwanja vya Ndege na kuongeza ushindano Afrika.