SERIKALI IMESISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI ZA BIDHAA

SIKU YA VIWANGO

     Serikali imesema inaendelea kusimamia sheria na kanuni kuhakikisha uzalishaji na uhamasishaji sahihi wa bidhaa unalindwa ili kumlinda Mtumiaji kutokana na mazingira.

    Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Viwango Afrika huko katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil, Kikwajuni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mhe: Sharif Ali Sharif amesema hatua hiyo itaziwezesha bidhaa zinazozalishwa Zanzibar kuingia katika ushindani wa Masoko kimataifa, hivyo amehimiza umuhimu wa kuimarisha utafiti wa bidhaa ili kubaini athari za bidhaa zisizo viwango.

    Akitoa Taarifa kuhusu Siku ya Viwango Afrika Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Viwango ZBS Ndg.Yussuf Majid Nassor amesema ZBS imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ikiwemo kutoa elimu ya viwango na uelewa ambapo hadi sasa wana idadi kubwa ya Watu waliowafikia.

    Nao Washindi wa Insha kuhusiana na viwango wameahidi eleza kuwa watakuwa Mabalozi wazuri kwa Jamii na kushajihisha matumizi sahihi za ubora wa bidhaa.

    Siku ya Viwango Afrika huadhimishwa kila ifikapo Tarehe 21/3/2024 ambapo Kauli mbiu inasema kuwa kuwawezesha Watumiaji kwa kupitia Viwango ili kupata haki zao za kupata huduma zenye ubora na usalama.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.