Nchi za Afrika zimetakiwa kuchukuwa hatua madhubuti za utunzaji wa Mazingira kwa kupanda Miti ili kuepuka Madhara yanayosababishwa na mabadiliko ya Tabia ya Nchi yakiwemo mafuriko yanayoharibu kingo za mito na kusababisha Mmomonyoko wa Ardhi
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la uhifadhi na usimamizi wa Mazingira Nchini (NEMC) Dkt. Immaculate Semesi wakati wa kupanda Miti 300 katika Pori la Pugu Kazimzumbwi Mkoani Pwani ikiwa ni Siku ya Mazingira Afrika na maadhimisho ya Siku ya Profesa Wangari maathai Raia wa Kenya Mwanaharakati wa mazingira aliyepewa tuzo ya Nobel Mwaka 1977 kutokana na juhudi hizo
Dkt Semesi amesema Mti ni mmoja ni Kiungo cha Dunia kinachoiwezesha kuishi kwani inaleta Hewa, Mvua, Chakula na kulinda Ardhi.
Naye Balozi wa Kenya Nchini Tanzania, Isaac Njenga amesema kila mmoja analo Deni na jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba ana Tunza mazingira kwa manufaa ya Kizazi kijacho.
Carolen Malunde ni Naibu kamishina wa uhifadhi kutoka Wakala wa huduma za misitu TFS na Abdul Juma Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Benki ya KCB Tanzania walikuwa na haya ya kusema.
Siku ya mazingira afrika huadhimishwa machi 3, kila mwaka ila Mwaka huu ilisogezwa Mbele kutokana na Msiba wa Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyekuwa Rais wa Pili wa Tanzania