Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Raisi Mh.Hamza Hassan Juma amezitaka Mamlaka za kudhibiti Maafa kuchukuwa hatuwa za haraka kwa Wananchi wanaojenga ujenzi holela.
Akizungumza katika Ziara ya kukaguwa Maeneo yalioathirika na Mvua Wilaya ya Magharibi "a" Mhe.Hamza amesema kufanya hivo kutanusuru Maafa ambayo husababishwa na Mvua na kupelekea kukosa Maakazi.
Amesema Serikali inafanya jitihada za makusudi ili kuweka usalama wa Wananchi wake dhidi ya Maafa mbalimbali hivyo kufuatia Ziara hiyo ametoa amri ya kuvunjwa misingi na nyumba zilizojengwa katika Mabonde ya Maji.
Wakaazi wa Bububu Kisimajongoo wameiomba Serikali kuwekea Mtoro ya Maji ili kuishi kwa salama kipindi cha Mvua za Masika
Wakati huohuo Waziri Hamza amefika katika Eneo lililoshambuliwa kwa kukatwa miti ovyo huko Mwera na kukuta miti ikiendelea kukatwa bila ya kufata taratibu za kisheria kwa lengo la kuuziana Viwanja vya kujengea Nyumba za Makaazi hivyo amezuia zoezi hilo na kuzitaka Mamlaka husika zichukuwe hatua.