KANDA YA ZIWA WAFIKIWA NA HUDUMA YA MAGONJWA YA MOYO

 Waziri Ummy Mwalimu

     Zaidi ya Watu Milioni 22 wa Kanda ya Ziwa wamerahisishiwa huduma ya Magonjwa ya Moyo na matibabu ya kibingwa kufuatia Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato.

     Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo Hospitalini hapo wakati wa Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi, huku akiweka bayana lengo la kuanzishwa kwa Hospitali hiyo.

     Daktari bingwa wa Uzazi na akina Mama Dk. Oswald Lyapa ametoa taarifa ya majengo yanayoendelea kujengwa Hospitalini hapo.
      Nae Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi, Mbunge kutoka Shinyanga Christina Mzava akashauri kwa upande wa Afya ya Mtoto kwa Mama mwenye maambukizi ya Ukimwi.
Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi na Mbunge kutoka Shinyanga,

    Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi, Stanslaus Nyongo amesema Kamati hiyo imeridhishwa na ujenzi huo na kuiomba Wizara kusaidia miradi ya afya kukamilika kwa wakati.

hot
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.