Jumla ya Watoto 400 wa Skuli ya Maandalizi ya Kidutani wamepatiwa huduma ya upimaji wa afya ili kuhakikisha wanakuwa na Afya njema
Zoezi hilo lililofanyika Skuli hapo, liliendeshwa na Timu ya Madakari wa kujitolea kutoka China ambapo Watoto hao walipatiwa Uchunguzi tofauti ikiwemo upimaji wa Macho, Masikio, Vinywa na Shindikizo la damu.
Akizungumza kwenye zoezi hilo, Mkuu wa Madakari kutoka China, Profesa Jiang Guoqing, alisema, lengo la upimaji afya ni jitihada za kuwasaidia Watoto kwa ajili ya kutambua afya zao na kupatiwa Matibabu watakapo gundulika na matatizo.
Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Maandalizi Kidutani Ndg.Asma Ali Yussuf, amesema zoezi hilo litawasaidia kutambua afya za Watoto hao na kuwaweka salama katika kuwajengea mustakabali bora wa masomo yao.
Nao baadhi ya Wazee wa Watoto hao wamelezea kufurahia kutolewa Huduma hiyo na kuiomba Serikali na Wizara ya Afya kuendelea kufanya zoezi hilo kila mara ili kuwaweka Watoto kwenye afya njema.
Timu ya ya 33 kutoka China wameendeleza ushirikiano na Zanzibar kwenye Sekta ya Afya kwa kutoka huduma za Afya kwa Jamii