Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Muhandisi Zena Ahmed Said amesema mfumo wa uombaji wa Vibali kwa njia ya Kidigitali kwa safari za Nje ya Nchi utaondosha upatikanaji wa Vibali kwa wakati Nchini.
Mhandisi Zena amesema hayo huko katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha Gombani Kisiwani Pemba wakati akifungua Mafunzo ya Siku Tatu ya kujenga uelewa wa juu matumizi ya Mfumo wa maombi ya Vibali vya Nje ya Nchi kwa Maafisa Wadhamini na Waratib wa Ofisi za Serikali Kisiwani Pemba.
Amesema Serikali imeamua kuanzisha mfumo huu ili kuondosha changamoto mbali mbali ambazo zinajitokeza kwa Watendaji ambazo zinawanyima fursa ya kupata Vibali kwa ajili ya kwenda kujifunza na kuboresha utendaji wao katika Kazi .
Mapema Afisa Mdhamin Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala bora Halima Khamis Ali amewataka Washiriki hao kujiandaa kutumia Mfumo huo kwa lengo la kupunguza Ghamarama na kurahisisha upatikanaji wa Vibali hivyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Serikali Mtandao Said Seif Said amesema kila mmoja anawajibu wa kuendana na mabadiliko hayo ya Kigitali katika kurahisisha utoaji wa huduma.