Ukosefu wa Elimu ya Mafunzo ya Ndoa husababisha migogoro kwa wanandoa na kuvunjika kwa Ndoa hizo
Akizungumza katika Mahafali ya 21 ya Mafunzo ya Ndoa Mjumbe kutoka Baraza la Maulamaa Sheikh Suwedi Ali Suwedi amesema Ndoa inahitaji Elimu ili kujenga uvumilivu na upendo kwa Wanandoa.
Amesema Mafunzo hayo yatasaidia kupunguza engezeko kubwa la Talaka na Migogoro hivyo amewataka Wanafunzi hao kufuata nasaha walizopewa na Walimu ili kudumu katika Ndoa zao.
Mgurugenzi usajili na usimamizi mambo ya Kiislamu Shekh Abdu Simba amesema Ofisi ya Mufti imeandaa Mafunzo hayo ili kupunguza Migogoro ya Ndoa na engezeko la Wajane.
Akisoma Risala Fatma Hassan Ali amesema wamejifunza mengi ikiwemo Mirathi kuishi kwa kustahamiliana pamoja na Uzazi wa mpango katika Uislamu.