Taasisi ya Uhasibu Tanzania TIA inaanzisha Mfumo mpya wa kuwasaidia Wanafunzi kusoma Mtandaoni nje ya Vituo vyao vya Masomo.
Akizungumza katika Mafunzo kwa Wakufunzi wa Taasisi ya uhasibu Tanzania (TIA), mratibu wa tathimini na ufuatiliaji Mradi wa HEET Magreth Emanuel amesema mradi huo umekusudia kuwafikishia Wanafunzi masomo kupitia Mtandao kwenye maeneo yoyote watakayokuwepo.
Mkuu wa Chuo cha Taasisi ya uhasibu Tanzania (TIA) Profesa William Pallangyo amesema Mradi huo wa HEET umehakikisha katika kipindi hiki ambacho Mitaala ya TIA unaisha muda wake, miitaala mipya inatakiwa kuwa ya Kimataifa zaidi.
Wakufunzi kutoka Taasisi ya uhasibu Tanzania (TIA) wamesema Mradi huo wa HEET utawasaidia Wanafunzi kupata huduma bora za kujisomea pamoja na kuhakikisha kuna kuwa na kipato endelevu kwa Mtu mmojammoja na kukuza Taasisi ya Uhasibu Tanzania.
Mfumo huu mpya ni Mapinduzi katika Taasisi ya uhasibu Tanzania tia ambao utawasaidia Wanafunzi kuondokana na tatizo la usomaji wa Masomo Mtandaoni, ambapo Mfumo huu umeletwa kupitia Mradi wa HEET ili kuhakikisha unaimarisha maeneo mbalimbali katika Taasisi hiyo.