KUTOKUWA WAKWELI KWA BAADHI YA MAWAKILI KUNAWACHAFULIA SIFA YAO

mawakili

     Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla amewataka Mawakili wa Serikali na wa kujitegemea kushirikiana katika kutatua matatizo yanayowakabili ili kuhakikisha Wananchi wanapata haki bila upendeleo wowote.

     Ameeleza hayo wakati akifungua kikao cha Mawakili wa Serikali na Mawakili wa kujitegemea huko Tunguu kwa lengo la kujadiliana namna ya kuyatafutia ufumbuzi matatizo na kujadili mafanikio katika Mwaka mpya wa Sheria 2024.

    Amesema kuwa pamoja Mawakili hao kunaweza kuleta mafanikio kwani kutasaidia upatikanaji mzuri wa haki na kuweza kuondoa matatizo baina yao na Mahkama.

     Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Mwanamkaa Abrahman ameushukuru Uongozi wa Mahkama kwa kuwaweka pamoja Wadau mbali mbali kwa lengo la kutafuta njia ya kuweza kuisaidia Jamii katika kupatikana kwa haki.

    Washiriki wa Mkutano huo wameeleza kuwepo kwa matatizo yanayohitaji kutatuliwa kwa haraka ikiwemo kutokufika Mahakamani kwa wakati, uwasilishaji wa maombi nje ya muda na kutokuwa wakweli kwa baadhi ya Mawakili jambo linaloweza kuwachafulia sifa Mawakili wengine.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.