KAMATI YABAINI UWEPO WA KASORO KWA BAADHI YA KANUNI

BARAZA LA WAWAKILISHI

Kamati ya kanuni na Sheria ndogo ndogo ya Baraza La Wawakilishi imesema imebaini baadhi ya Kanuni kuwa na kasoro ikiwemo kuandikwa bila ya kuzingatia Vifungu wezeshi katika Sheria husika.

Akiwasilisha Ripoti ya Kamati Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Mihayo Juma N'hunga amezitaja kasoro nyengine ni baadhi ya Kanuni kuwasilishwa katika kamati bila kutangazwa katika Gazeti rasmi la Serikali jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Akizungumzia dhana ya baadhi ya maneno kupishana na uhalisia na miongozo Mh N'hunga amesema Sheria na Kanuni. Lazima ziendane na uhalisia na kutotoa mtazamo nje ya uhalisia ikiwemo Zao la Miwa kuhesabiwa kwa mtazamo wa Matuta.

Wajumbe wa Baraza La Wawakilishi wakichangia Ripoti hiyo wamesema ipo haja ya kubadilishwa kwa Sheria za malipo ya vipando ili iendane na Gharama za Miti na Mazao yenyewe.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.