VETA NA KIST ZAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe Leila Mohamed Mussa amesema Serikali imekusudia kuzalisha Walimu wenye viwango kupitia ufundi na Mafunzo ya Amali. 

Waziri Lela ametoa Kauli hiyo, katika utiaji Saini kati ya Taasisi ya Sayansi na Ufundi (KARUME) na Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) kwa lengo la kukuza na kuzalisha Walimu wapya wenye uwezo wa kufundisha ufundi na Mafuzo ya Amali.

Mh: Lela amezipongeza Taasisi zote mbili na amesema hatua hiyo itasaidia kukuza umoja na ushirikiano kati ya Bara na Visiwani.

Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Elimu na ufundi stadi (veta) Dkt. Prosper Mgaya amesema mabadiliko ya mfumo wa Elimu unahitaji idadi kubwa ya Walimu wa stadi za ufundi na kueleza umuhimu wa Mkataba huo.

Mkurugenzi Taasisi ya Sayansi na Ufundi (karume) Dkt. Mahmoud Abdulwahid amesema Chuo cha Karume kipo Mstari wa mbele kuendana na mabadiliko ya mfumo wa Elimu, hivyo makubaliano hayo yataleta chachu ya mabadiliko ya Taasisi hizo.

Makubaliano hayo kati ya Veta na Taasisi ya Karume (KIST) ni ya ushirikiano wa kukuza wigo wa Taaluma na kuzalisha Walimu wenye uwezo wa kufundisha kupitia Mafunzo ya Amali.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.