Kamati ya Utalii Biashara na Kilimo imesema imesikitishwa na kitendo cha Mamlaka za Serikali za Mitaa kushindwa kutekeleza matakwa ya Kisheria ya kuipatia Wakala wa Uwezeshaji Kiuchumi asilimia 10 ya Pato la ndani linalokusanywa na Mamlaka hizo.
Akiwasilisha Ripoti ya Kamati hiyo Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Mtumwa Pea Yussuph amesema hali hiyo inapelekea maombi mengi kutoka kwa makundi hayo kukosa mikopo kutokana. na. Uhaba wa Fedha.
Ripoti hiyo imeeleza kusikitiswa kwa kutokamilika kwa wakati Ujenzi Wa Kiwanda cha kusarifu Dagaa. Kilichopo kama. Ambapo ilitarajiwa mradi huo uwe umekamilika kwa asilimia 100 ifikapo Disemba 2023.
Wakichangia ripoti hiyo Wajumbe hao wameiomba Serikali kukaa na Wafanya Biashara ili kuona Bei za Bidhaa zinapunguzwa ili kuwasaidia Wananchi ambao ni wanyinge na wenye kipato cha chini ili kumiliki Gharama za Bei hizo.