Mkuu wa Wilaya ya Kusini Galos Nyimbo amewahimiza Wananchi kuendelea kuweka Mji katika hali ya usafi kufanya hivyo utaongeza idadi ya Watalii kuitembelea Zanzibar.
Akizungumza katika usafi wa mazingira huko Michamvi ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Familia ya Polisi . Polisi Familly Day amesema Jeshi la Polisi ni Sehemu ya Jamii, hivyo kufanya usafi itaishajihisha Jamii kuhifadhi na kutunza Mazingira ambayo ni miongoni mwa vivutio vya Wageni katika Fukwe.
Mwengine ameliomba Jeshi la Polisi kupitia Chuo cha Polisi Zanzibar kutoa Mafunzo maalum kwa Walinzi wa Kampuni Binafsi ili kuwajengea uwezo katika kazi zao na kuifanya Jamii kuendelea kua salama
Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi Augostino Senga amesema wameamua kuadhimisha Siku hiyo kwa kufanya usafi kwa kushirikiana na Wananchi ili kuwaweka Karibu na kuendelea kushirikiana nao katika mambo mbali mbali.
Afisa wa Mazingira Wilaya ya Kusini Unguja Ndg. Ramadhani Haji Ameir ameiomba Jamii kuhakikisha inatunza mazingira yanayo wazunguka ili kujiepusha na Maradhi ya Mripuko.