VIASHIRIA VYA IDADI YA WATU NI MSINGI WA MAENDELEO

MAAFISA MIPANGO

    Maafisa mipango wamehimizwa kuangalia viashiria vya idadi ya Watu katika kutoa maamuzi wakati wa utekelezaji wa mipango yao ili Serikali iweze kupanga Bajeti yake kwa usahihi.

    Wito huo umetolewa na Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar Ndg.Rahma Salum Mahfudh alipofungua Mafunzo kwa Maafisa mipango hao juu ya uwingizaji wa viashiria vya idadi ya Watu katika mipango na Bajeti huku Mazizini ,Amesema ni muhimu kujua viashiria vya idadi ya Watu ambao ndio msingi katika kufikia malengo ya maendeleo.

    Kamishna Idara ya Mipango na maendeleo watendaji kazi Dkt. Rukkaya Wakif Muhammed amefahamisha kuwa ili kuweza kupanga mikakati mizuri ambayo itayokuwa endelevu wameona ipo haja ya kutoa Mafunzo hayo kwa Maafisa kujua wanapotengeneza mipango katika Sekta zao kuhakikisha viashiria hivyo wanaviangalia.
    Wakufuzi kutoka Chuo cha Mipango ya Maendeleo Dodoma Ndg.Hamenya Kasesa na Dkt Maseke Mgabo wamesema upo umuhimu wa kutumia viashiria vya idadi ya Watu kwa lengo la kufanikisha mipango ya Nchi.

    Nao Maafisa mipango kutoka Taasisi mbalibali za SMZ wamesema  Mafunzo hayo yatawajengea misingi imara ndani ya Sekta zao na kuyafanyia kazi kwa ufanisi. 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.