Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewataka Viongozi wa Serikali, Sekta Binafsi na Wadau wa maendeleo Nchini kuweka mikakati ya pamoja ya kujenga miundombinu ya Tehama na kuandaa program za kuwawezesha Vijana ili kupunguza utegemezi.
Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati wa Mkutano wa Future Ready Summit liloandaliwa na Kampuni ya Mtandao wa Vodacom uliyowakutanisha Wafanyabiashara, Wabunifu Chipukizi na Wadau wa Teknolojia wa ndani na nje ya Nchi amesema Serikali inatarajia kuazisha Ujenzi wa Chuo maalum kitakachosaidia Vijana kusoma kidijitali ili waweze kufanya Biashara zao na mambo mbalimbali.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mhe. Nape Nnauye amesema Serikali kupitia Wizara hiyo imejipanga kukuza Tehema kwa kuhakikisha kazi ya Mapinduzi ya Teknolojia ya Viwanda yanaenda vizuri.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Vodacom Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema lengo la Mkutano huo ni kuwawezesha Vijana hasa wa Kike katika kutatua matatizo ya Biashara zisizofaa kwa kutumia mitandao katika matokeo chanya.