KUWEPO SHERIA YA MAMLAKA SERIKALI MTANDAO KUTAONGEZA UFANISI

MHE.HAROUN ALI SULEIMAN

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria utumishi na utawala bora Mhe Haroun Ali Suleiman amesema lengo la kutungwa Sheria ya Mamlaka ya Serikali Mtandao ni kuweka usimamizi wa masuala ya Teknologia ya Habari na Mawasiliano katika Utumishi wa Umma.

Akiwasilisha mswada wa kufuata Sheria ya Wakala Serikali mtandao No.12 ya Mwaka 2019 na kutunga Sheria ya Mamlaka ya Serikali Mtandao Zanzibar amesema Sheria hiyo itawezesha  kuweka utaratibu mzuri wa uanzishwaji na uwendeshaji wa mifumo ya Kieletronic Nchini.

Akisoma maoni ya Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Mariam Thani juma amesema kamati inasisitiza juu ya kujenga Mazingira wezeshi ya kisheria kwa ajili ya kuratibu usimamizi na uwendeshaji wa matumizi ya TEHAMA ili kuimarisha utowaji wa huduma za Serikali kwa Umma.

Wakichangia Muhtasar wa mswaada huo  Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamesema kupatikana kwa Sheria ya Mamlaka ya Serikali Mtandao itawezesha Serikali   kuwa na Chombo madhubuti cha uwendeshaji  wa shughuli zake Kidigital   

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi   kwa pamoja wameupitisha Mswaada wa huo

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.