WATOTO WATAKIWA KUPEWA CHAKULA KULINGANA NA UMRI WAO

lishe

     Jamii imetakiwa kuwa na utaratibu  wa kuwapa chakula Watoto kulingana na umri wao ili kuwakinga na maradhi ya utapia mlo.

    Akizungumza katika kazi ya upimaji wa  Afya kwa Watoto na  kutoa elimu kwa Jamii juu ya umuhimu wa kula Vyakula vyenye lishe Diwani wa kuteuliwa Wilaya ya Kaskazini 'b'Ndg.Fatma Suleiman Ukindu Amesema kwa mujibu wa Wataalamu wa Afya Wilaya hiyo ni miongoni mwa Wilaya zenye Watoto wenye Utapia mlo hivyo katika kuliona hilo Madaktari wamelazimika kupita kila Shehia kwa kushirikiana na Wahudumu wa Afya wa Jamii ili kuwasogezea huduma karibu na kuwapima afya Watoto zao. 

    Muuguzi Mkunga kutoka Kituo cha Afya Mahonda Ndg.Mwanaasha Othman Omar na Katibu wa Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii Wilaya ya Kaskazini 'b' Ndg.Fatma Masoud Said wamewataka Wananchi wa Wilaya hiyo kuwacha tabia ya kutumia dawa kiholela na badala yake kufika Vituo vya afya na kutoa ushirikiano pindi huduma za afya zinapofika katika Shehia zao ili kupata matibabu.

    Wananchi waliopatiwa matibabu wameishukuru Serikali kwa kuendeleza utaratibu wa kuwasogezea huduma za afya Vijijini.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.