Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan. Amesema Tanzania itaendeleza ushirikiano na Taifa la Poland katika mipango ya maendeleo kupitia Sekta za kimkakati zikiwemo Biashara na uwekezaji.
Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mapokezi rasmi na kuwa na mazungumzo ya faragha na Rais wa Poland Andrezej Duda aliewasili Nchini jana Raisi Samia amesema Ziara ya Rais duda ni kielelzo cha kuimarisha fursa za uwekezaji katika Sekta za Tehama, Kilimo, Utalii, Usimamizi wa Taka Uchumi wa Kidigitali na Uchumi wa Buluu.
Rais Samia amewashajihisha Wawekezaji wa Poland kuangalia fursa zilizopo Tanzania na kuja kuwekeza katika Sekta ya Utalii hususani Ujenzi wa Hoteli za Utalii.
Ameainisha kuwa uwiano wa biashara kati ya Tanzania na Poland ni mdogo hivyo upo umuhimu wa kukuza biashara ikiwa ni hatua ya kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia.
Kwa upande wake Rais wa Poland Andrezej Duda amesema Nnchi yake ipo tayari kuisaidia Ttanzania kupitia uwekezaji katika Sekta za Ujenzi wa Viwanda vya Kisasa, Mifumo ya Kibenki, Kilimo, Ujenzi wa Miji, Elimu na Tehama.
Akizungumzia Sekta ya Utalii Rais Duda amesema hali ya Uchumi wa Wananchi wa Taifa lake kwa sasa ipo vizuri na hivyo watatumia fursa ya kuja kutalii Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Poland ni Taifa la 21 kwa ukubwa wa Uchumi Duniani na uhusianao kati ya Tanzania na Poland umeimarika kwa kiasi kikubwa baada ya kubadilishwa kwa Sera ya Mambo ya Nje ya Poland iliyolenga kuanzisha na kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na Nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania