SMT NA CUBA ZIMESAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO

MAKAMO WA RAIS WA TANZANIA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamuhuri ya Cuba zimesaini makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya Kilimo, Afya, na Elimu ili kuongeza tija ikiwemo kukiongezea nguvu Kiwanda cha kuzalisha Dawa za kuulia Wadudu kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani.

Makubaliano hayo yamesainiwa Jijini Dar Es Salaam na wawakilishi wa Tanzania na Cuba na kushuhudiwa na Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt Philip Mpango na Makamo wa Rais wa Cuba Salvador Veldes ikiwa ni sehemu ya ziara ya Kiongozi huo Nchini.

Akizungumza mara baada ya kutiliana saini makubaliano hayo Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Philip Mpango amesema makubaliano hayo yana umuhimu mkubwa katika Nchi sababu yanaenda kuongeza ushirikiano baina ya Mataifa hayo.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh Salvador Veldes Mesa amesema Cuba itaendelea kushirikiana na Tanzania kwasababu wana mahusiano ya muda mrefu tangu uongozi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mataifa hayo mawili yaliasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa upande wa Tanzania na kwa upande wa Cuba Fidel Castro Mwaka 1962.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.