Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Hassan Khamis Hafidha amesema hali ya Vifo vya Mama na Watoto imekuwa tatizo Nchini kutokana na ukosefu wa Damu kwa Mama Mjamzito wakati wa kujifungua na kutohudhuria Kilini kwa wakati.
Akizungumza katika Mkutano maalum wa kutathimini Vifo vya Mama Wajawazito kati ya Wizara na Watendaji mbali mbali wa ndani na Nje ya Nchi Naibu Hafidhi amewataka kina Mama hao kutumia Lishe bora ili kuwa na kiwango sahihi cha Damu ambacho kitaweza kumsaidia wakati wa kujiifungua.
Meneja Kitengo Shirikiahi cha Afya ya Uzazi na Mtoto Dk Camilia Ali Omar amesema ni vyema kuhakikisha tatizo la Vifo linapungua katika kipindi cha Mwaka 2024 na kufikia 70 juu ya 70 ifikapo 2030.
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga na Elimu ya Afya Dk Salim Muhamed Slim amesema Serikali kwa kushirikiana na Wadau wanakusudia kumgusa Mzanzibar ili kuimarisha afya zao.
Mshiriki wa Mkutano huo Azzah Amin Nofli amewashauri kina Mama kuhudhuria Vituo vya afya watakapokuwa Wajawazito na kuzingatiwa Lishe bora.