Akizungumza Katika Kikao Kazi Cha Wataalamu Na Wadau Wa Utalii Katibu Mkuu Wizara Ya Utalii Na Mambo Ya Kale Fatma Mbarouk Khamis, Amesema Lengo La Utafiti Huo Wa ZTCC Ni Kutathmini Uwezo Wa Zanzibar Wa Kuhimili Watalii Wanaoingia Nchini Pasipo Kuleta Madhara Yoyote Kwa Nchi Na Wananchi.
Mshauri Elekezi Wa Wizara Ya Utalii Na Mambo Ya Kale Prof. Haji Semboja Na Kiongozi Wa Mradi Huo Prof. Jumanne Abdallah, Wamesema Kuna Ongezeko La Utalii Wa Ndani Na Wageni Kutoka Nchi Mbali Mbali Duniani Hivyo Kufanyika Kwa Utafiti Huo Kutasaidia Kupata Maoni Ya Wadau, Wananchi Na Wataalamu Juu Ya Namna Ya Kuimarisha Huduma Na Miundombinu Ili Nchi Iendelee Kuwa Salama.
Mkurugenzi Mtendaji Wa Kampuni Binafsi Ya Africom Limited Ambayo Ni Washauri Elekezi Wa Mradi Wa Utafiti Wa Zanzibar Tourism Carrying Capacity (ZTCC), Kassim Abdi Kassim Ameishukuru Serikali Kwa Kuiamini Africom Na Kuahidi Kusimamia Vyema Mradi Huo, Ili Uweze Kuleta Matokeo Chanya Na Kufikia Malengo Yaliyokusudiwa.
Washiriki Wa Kikao Hicho Wamewashauri Wataalamu Hao Kuyatizama Kwa Kina Maeneo Ambayo Bado Hayapo Vizuri Katika Sekta Hiyo, Kwa Lengo La Kuyaimarisha Ili Wageni Wanapokuja Nchini Waweze Kufurahia Vivutio Na Huduma Za Kitalii.
Takwimu Za 2023 Zinaonesha Kuwa Zaidi Ya Watalii Laki Tano Wameingia Nchini Na Kuchangia Asilimia 80 Ya Pato La Fedha Za Kigeni Na Asilimia 35 Ya Wafanyakazi Katika Sekta Hiyo.