WANANCHI WANAONG’OA VIBANGO VYA UTAMBULISHO WA MAJINA YA MITAA NA NAMBA ZA NYUMBA KUWACHA TABIA HIYO.

MH. KASSIM MAJALIWA

Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makaazi ya Mwaka 2022 Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameyasema hayo katika Kikao cha kumi 10  cha Kamati Kuu ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makaazi ya Mwaka 2022 Mhe Majaaliwa amesema Tamisemi kwa pande zote mbili zina wajibu wa  kufuatilia  na kuhakikisha Vibao vya Anuani za Majina ya Mitaa havibanduliwi na vinabaki katika uhalisia ili kumrahisishia Mwananchi kufika sehemu husika bila ya usumbufu wa aina yoyote.

Waziri Mkuu amezitaka Serikali za Mitaa kuhakikisha wanapotoa vibali vya Ujenzi kwa Wananchi vitolewe  pamoja na namba za Nyumba ili kurahisisha upatikanaji wa maendeleo kwa Wananchi na kuirahisishia Serikali kufikia malengo ya kuwapatia huduma muhimu Wananchi kupitia Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi.

Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Kuu ya Sensa ya Watu na Makaazi ya mwaka 2022 ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali imeridhika na viongozi wa SMT kufanikisha sherehe za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar jambo  linalodhihirisha uimara wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Aidha amewataka Viongozi kuwa msari wa mbele katika kuzisaidia Serikali zote mbili katika kuleta  mabadiliko ya Kimaendeleo kwa Wananchi wake kupitia Tawimu za Sensa ya Watu na Makaazi Mjini na Vijijini.

Wajumbe wa kamati kuu ya sensa ya mwaka 2022  wamezitaka Tume zote mbili za Uchaguzi kuhakikisha zinayatumia matokeo ya Sensa kwa ajili Daftari la Wapiga Kura ili Watu wote wenye sifa za kupiga Kura waweze kuandikishwa na kupata haki yao ya msingi.

Kamati hiyo imedhamiria kuhakikisha Wizara, Idara na Taasisi za Serikali zinapeleka mahitaji yao ya Takwimu za kisekta zilizotokana na Sensa ya Watu na Makaazi katika Ofisi za Takwimu kwa ajili ya kufanya uchambuzi wa kina utakaotoa maamuzi yenya Tija.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.