ZAIDI YA WAGENI 2000 KUTOKA NCHI MBALI MBALI DUNIANI WAMEWASILI NCHINI KWA LENGO LA KUTALII KUPITIA MELI KUBWA YA NORWEGIAN DAWN IKITOKEA KENYA NA KUELEKEA DAR ES SALAAM.

WATALII

Akizungumza Na Vyombo Vya Habari Katika Meli Hiyo, Waziri Wa Utalii Na Mambo Ya Kale Mhe. Simai Mohamed Said, Amesema Malengo Ya Serikali Ya Kuitangaza Zanzibar Kiutalii Yanafanikiwa Kutokana Na Kuwasili Kwa Meli Za Kimataifa Hatua Inayochangia Kukuza Pato La Taifa. 

 

Kepten Wa Meli Hiyo Asen Gyruv, Amesema Wamevutiwa Kuja Kutembea Zanzibar Kutokana Na Uzuri Wa Mandhari Yake Ya Asili Na Ukarimu Wa Watu Wake, Na Kuahidi Kuifanya Zanzibar Kuwa Miongoni Mwa Vituo Vya Kushusha Abiria.

 

Kamishna Wa Uhamiaji Zanzibar Hassan Ali Hassan Na Mwenyekiti Wa Kamisheni Ya Utalii Zanzibar Rahim Baloo, Wameahidi Kuhakikisha Wanatoa Huduma Bora Kwa Wageni Ili Kuweza Kuwa Mabalozi Wazuri Wa Kuitangaza Zanzibar.

 

Meli Ya Norwegian Cruise Line Imewasili Zanzibar Kwa Ziara Ya Siku Moja Ikiwa Na Abiria 2214 Na Mabaharia 1013. 

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.