ASASI ZA KIRAIA ZIMESHAURIWA KUOMBA MIRADI KWENYE SHIRIKA LA DANMISSION

ASASI ZA KIRAIA

Asasi Za Kiraia Zanzibar Zimetakiwa Kutumia Fursa Zinazotolewa Na Mashirikaka Ya Nje Katika Kutekeleza Miradi Yao Ya Kusaidia Jamii.

 

Mrajis Wa Asasi Hizo Ahmed Khalid Abdullah Ameeleza Hayo Katika Mkutano Wa Kulitambulisha Shirika La Danmission, Lenye Lengo La Kutoa Ufadhili Wa Miradi Kwa Asasi Za Zanzibar, Amesema Ni Vyema  Kwa Asasi Zikatumia Fursa Za Ufadhili Wa Miradi Zinazotolewa Na Shirika Hilo.

 

Mkurugenzi Mkuu Wa Danmission Tais Kroger Ziethen, Amesema Shirika Hilo Lipo Tayari Kufadhili Miradi Ya Amani Na Uhifadhi Wa Mazingira Iliyomo Ndani Ya Asasi Za Kiraia Zilizo Sajiliwa Zanzibar Ndani Ya Miaka Mitano.

 

Washiriki Wa Mkutano Huo Wameahidi Kuomba Miradi Katika Shirika Hilo Kwa Fursa Hiyo Waliokuwa Wakiihitaji.

 

Asasi Za Kiraia Zanzibar Zimekuwa Zikifanyakazi Za Kuisaidia Serikali Katika Kufikia Maendeleo Hasa Kwenye Sekta Ya Elimu, Maji Safi Na Salama Pamoja Na Uhifadji Wa Mazingira Na Mabadiliko Ya Tabia Nchi.

 

       

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.