KUIMARIKA KWA BIMA KUTALETA USHINDANI SOKO LA BIASHARA

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO

Kuimarika kwa huduma bora za Bima Zanzibar kutazidi kuleta maendeleo kwa Wananchi wake.

 Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa muonekano mpya wa Shirika la Bima Zanzibar ZIC Waziri Ofisi ya Rais fedha na mipango Dk Sada Mkuya Salum amesema hatua hiyo itazidi kuimarisha ushindani katika Soko la kibiashara amesema Mapinduzi ya Kiuchumi Zanzibar yanalengo la kuleta maendeleo kwa Wananchi wake huku akizidi kutoa wito kwa Jamii kukata bima kwa maslahi ya mali zao.

Mkurugenzi muendeshaji wa Shirika La Bima Zanzibar Arafat    amesema mabadiliko hayo yanalengo la kuboresha huduma za bima kwa wateja  katika nyanja mbalimbali ndani na Nje ya Nchi amesema Shirika hilo kwa Miaka mitatu ya awamu ya nane ya Serikali limeweza kukusanya mapato ya Shilingi Bilioni 45 kutoka wastani wa bilioni20 Mwaka wa 2020.

Balozi wa bima Mh Wanu Hafidh Ameir amehimiza utowaji wa Elimu ya Bima kwa Wananchi ili waweze kunufaika na bima hiyo huku akisisitiza kuzidi kasi za utoaji wa huduma bora za Bima.

Muonekano mpya wa ZIC ambao umebeba ujumbe wa muonekano mpya huduma bora zaid.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.