Sherehe Za Kuwatunuku Nishani Viongozi Hao Zimefanyika Katika Viwanja Vya Ikulu Mjini Zanzibar Katika Maadhimisho Ya Miaka 60 Ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt Mwinyi Amemtunuku Nishani Ya Mapinduzi Ya Kiongozi Mwenye Sifa Ya Kipekee Rais Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzani Dkt Samia Suluhu Hassan.
Nishani Nyengine Ni Viongozi Na Wananchi Wenye Sifa Maalum Ambapo Dkt Muhamed Gharib Bilal, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, Balozi Seif Ali Iddi Na Marehemu Seif Sharif Hamad Wamekabidhiwa Nishani Hizo.
Wengine Ni Utumishi Uliotukuka Imekabidhiwa Kwa Dkt. Abdul Hamid Yahya Mzee, Saleh Idirisa Na Salum Faki Hamad.
Nishani Ya Utumishi Wa Muda Mrefu Na Utalii Kwa Idara Maalum Za Smz Imetunukiwa Kwa Muhamed Suleiman Haji, Mohamed Salum, Mariam Kurwa Na Luteni Kanal Khadija Ahmada.
Nishani Ya Ushujaa Imetunikiwa Kwa Marehemu Khalid Abas, Dkt. Suleiman Maulid Mussa.
Kwa Namna Moja Ama Nyengine, Waliotunukiwa Nishani Hizo Wamekuwa Na Mchango Mkubwa Katika Kuyalinda Mapinduzi Ya Zanzibar Pamoja Na Utendaji Kazi.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi Ya Rais Ali Salum Akisoma Wasimu Wa Dkt. Samia Amesema Aliwahi Kuwa Mwanamke Wa Kwanza Kuwa Makamu Wa Rais Na Hivi Sasa Ni Rais Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania.
Baadhi Ya Waliotunukiwa Nishani Hizo Wakizungumza Na Zbc Wamesema Wanaishukuru Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Kwa Kuthamini Mchango Wao.