Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Nchi inaendelea kuimarisha huduma za afya ikiwa ni miongoni mwa dhamira ya Mapinduzi ya mwaka 1964.
Akizungumza wakati alipozinduwa Hospitali ya Mkoa wa Mjini Magharibi huko Lumumbakatika shamra shamra za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Samia amesema kwa vile Hospitali hiyo itatoa huduma bora na za kisasa ni vyema watendaji na wahusika wa hospitali kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa Wananchi zinaimarika kuwa bora zaidi.
Aidha Dkt samia amewatoa wasiwasi Wananchi kuwa Hospitali hiyo haina tofauti na Hospitali nyengine ikiwemo india katika ubora wa Vifaa na huduma zilizokuwemo.
Waziri wa Afya Mhe Nassor Ahmed Mazrui amesema Serikali imejenga Hospitali 10 za Wilaya ikiwa ni juhudi za Viongozi wakuu wa Nchi hivyo amewataka Wafanyakazi kushirikiana katika kazi zao ili kufikia lengo la kutoa huduma bora na salama.
Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dkt Amour Suleiman amesema Mradi huo umegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 32 ambazo ni fedha za uviko 19 na Hospital hiyo itatoa huduma za Mama na Mtoto, Maradhi ya Damu, Moyo, huduma za Kibingwa pamoja na kuweza kuwahudumia Wagonjwa kutoka maeneo mbali mbali.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Idrisa Kitwana Mustafa amempongeza Dkt samia kwa kuliongoza Taifa katika hali ya amani na utulivu.