Michezo

NEW CITY YAJIPANGA KUMALIZA NAFASI ZA JUU LIGI KUU YA PBZ

    New Ccity inayocheza  Ligi Kuu Zanzibar imetoa Mapumziko ya Mwezi kwa Wachezaji  kwa ajili ya kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hadi  baada ya Ramadhani

    Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Ndg.Suleiman Salum ambae pia ni Mwenyekiti

wa Bodi ya Ligi Zanzibar, amesema wameamua kutoa Mapumziko kwa Wachezaji wao ili wapate muda wa kupumzika kujiandaa

kuipambania Timu watakaporudi.

     Kuhusu suala la kumaliza ligi nafasi za juu, Mwenyekiti amesema malengo yao ni kumaliza nafasi ya juu na kujinusuru kushuka

ZIFF YAPATA VIONGOZI WAPYA

    Tamasha la Kimataifa la Filam la Zanzibar ZIFF limepata Viongozi wapya na  kuahidi kuleta mabadiliko na ufanisi katika kazi  .

    Akizungumza katika Mkutano huko Maru Maru Makamo Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filam la Zanzibar ZIFF Ndg. Thani Mfamau amesema wameamua kuchagua Viongozi wapya watakao ongoza Tamasha la Filam la Zanzibar ili kuleta mabadiliko  katika kazi pamoja  na kutekeleza  Majukumu yao vizuri..

LIGI KUU WANAWAKE YASIMAMA KUPISHA RAMADHAN

    Katibu Kamati ya Soka la Wanawake Zanzibar, Ndg.Neema Othman Machano amesema Ligi kuu ya Wanawake inasimama kupisha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na itaendelea mzunguko wa Pili baada ya Ramadhan.

     Katibu amesema kwa sasa wapo vizuri, wanaiomba Serikali na Shirikisho kuwawezesha Makocha wa Kike kujifunza na

kuongoza Timu za Wanawake.

     Amesema muamko wa Wanawake kujitokeza kujifunza ni mdogo kwani wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mbali mbali

ikiwemo uhaba wa Ffedha.

MICHUANO YA POLISI JAMII KUTIMUA VUMBI MWEZI JUNI

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud amesema Serikali ya Mkoa itaendelea kuunga Mkono Michezo ili kusaidia kurejesha hadhi ya Michezo katika Mkoa huo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo kwenye Kikao maalum kuelekea mashindano ya Polisi Jamii ya Mkoa, huko kwenye Ukumbi wa Skuli ya Michamvi, Mkuu wa Wilaya ya Kusini Gallos Nyimbo amesema Michezo inanafasi kubwa ya kuwapa Ajira Vijana ili kukuza Vipaji na kukuza uchumia wa wana Michezo.

IDARA YA MICHEZO YAAHIDI KUENDELEZA VIPAJI

      Idara ya Michezo na Utamaduni kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, imesema itaviendeleza vipaji vya Watoto vilivyopatikana kwenye mbio za nyika.

     Akizungumza katika mbio za nyika (Elimu Cross Country) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Mnazi Mmoja, Mkurugenzi Idara ya Michezo na Utamaduni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ndg.Abdalla Mussa amesema Mashindano hayo yatapelekea kujenga afya za Watoto hao na kuangalia vipaji ambavyo wapo navyo ili wapate kuviendeleza.

MAKUBWA YAFANYWA NA KIKUNDI CHA MAZOEZI CHA ZONE "A"

     Zaidi ya Shilingi Milioni Moja zimekusanywa na Vikundi vya Mazoezi Zone 'A' katika Harambee ya kuchangia Wanachama wa Zoni hiyo wanaoishi katika Mazingira magumu na Yatima.

    Fedha hizo zimepatikana baada ya Vikundi hivyo vya Mazoezi kufanya Matembezi kuanzia Kisonge hadi Viwanja vya  

Mao -ze -dong na kufanya Mazoezi pamoja na Harambe itakayosaidia kupata huduma Wanachama wao katika Mwezi wa Ramadhani.

KIKUNDI CHA MAZOEZI ZONE 'A' WAANDA HARAMBEE KWA WAJNE NA YATIMA

    Wananchi wamehimizwa kuendelea kufanya mazoezi na kusaidiana katika Kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kutekeleza Ibada na Fadhila za Allah.

     Katibu wa vikundi hivyo vya Mazoezi Zone 'a' Ndg. Suleiman Sichwale amesema Jumapili Machi 10, wameandaa Mazoezi na Harambee ya kuchangia Wajane ,Yatima na Wanaoishi mazingira magumu katika  kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

KIPIGO KIZITO CHAKIPATA ZBC

     Mashindano ya May Day yameanza kwa kishindo kwenye Viwanja vya Mao -Zedong kati ya ZBC dhidi ya Mnazi Mmoja.

      Mchezo huo uliochezwa Jioni ya Leo katika Uwanja wa Mao 'b' na kushuhudiwa na Washabiki  wa soka, Timu ya ZBC imeshindwa kuonyesha makali yake baada ya kuwakosa Wachezaji wake Mahiri akiwemo Mzee Yussuf na Salum Ramadhan jambo ambalo liliwafanya Madaktari wa Mnazi mmoja kutoka kifua mbele na kuibuka mshindi katika Mtanange huo wa Ufunguza wa Mashindano hayo.

SIMBA SC YAWASILI IVORY COAST

    Kikosi cha Wachezaji wa Simba, kimeondoka leo Alfajiri kuelekeza Ivory Coast kwa ajili ya Mchezo ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi utakaochezwa Ijumaa ijayo.

     Akieleza umuhimu wa Mchezo huo kabla ya kuodoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Beki wa Timu hiyo David Kameta Duchu amesema Wachezaji wote wana hamasa ya kushinda mchezo huo.

KILIMO BINGWA MBELE YA TRA

    Timu   ya Kilimo imetwaa ubingwa  mashindano ya ligi za  Mawizara baada kuiadhibu TRA  kwa Mikwaju ya  Penalt 3-1.

    Fainali  hiyo iliyokua ya aina yake  Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1  baada ya Dakika  90  kumalizika  ikafuata  hatua  mikwaju ya Penalt.

    Kepteni wa Timu hizo wamesema  michezo hiyo  inahamasa kubwa na inasaidia kuunganisha  Wafanyakazi wa Wizara na Taasisi za Umma

Subscribe to Michezo
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.