New Ccity inayocheza Ligi Kuu Zanzibar imetoa Mapumziko ya Mwezi kwa Wachezaji kwa ajili ya kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hadi baada ya Ramadhani
Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Ndg.Suleiman Salum ambae pia ni Mwenyekiti
wa Bodi ya Ligi Zanzibar, amesema wameamua kutoa Mapumziko kwa Wachezaji wao ili wapate muda wa kupumzika kujiandaa
kuipambania Timu watakaporudi.
Kuhusu suala la kumaliza ligi nafasi za juu, Mwenyekiti amesema malengo yao ni kumaliza nafasi ya juu na kujinusuru kushuka
Daraja.
New City ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na Alama 22 akiwa amecheza Michezo 20.
stories
standard