WATU WATATU WAFARIKI DODOMA LORI ZAGONGANA USO KWA USO

AJALI
English

Watu watatu wamefariki dunia kufuatia ajali ya barabarani iliyohusisha malori mawili yaliyogongana uso kwa uso katika mtaa wa Emaus, eneo la Mataa ya Waziri Mkuu, jijini Dodoma, saa kumi na mbili asubuhi ya leo Aprili 29, 2026.

Akizingumza na vyombo vya habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi Dodoma, Gallus Hyera, amesema kuwa ajali hiyo imehusisha lori lenye namba za usajili T 764 EPW lililokuwa limebeba saruji, pamoja na lori lenye namba T 179 EQF lililokuwa limebeba mchanga.

Taarifa za awali za kamanda Gallus zinasema chanzo chs ajali hiyo ni Usingizi wa Dereva aliyakuwa amebeba shehena ya sarufi ambae ndie chanzo cha ajali hiyo.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa  Dodoma, RJ Menda amethibitisha kutokea kwa tukio hilo majira ya saa moja asubuhi Ambapo Amesema baada ya kufika eneo la tukio walikuta gari Zote mbili zikiwa zinawaka moto.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.