Chama cha Mapinduzi,(CCM) Mkoa wa Tanga kimeagiza kufuatiliwa na kuthibitishwa vikundi vyote vya Vijana,Wanawake na wenye Ulemavu katika Jiji la Tanga,ili kuweza kujua uhalali wake.
Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdallah wakati kukabidhi pikipiki katika vikundi vya Vijana katika eneo la Kirare jijini Tanga April Mosi,2026 na kumuagiza Mwenyekiti wa UVCCM mkoa afuatilia kujua uhalali wake.
Afisa Vijana Jiji la Tanga Fadhili Secha amesema kuwa jumla ya Vikundi 319 vya wanawake,vijana na wenye ulemavu vimenufaika kwa kupata mikopo kwa nyakati tofauti na kufanya kuweza kuendesha shughuli zao za kiuchumi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi,(UVCCM) Mkoa wa Tanga Ramadhani Omari amewashauri vijana kuendelea kuwa wabunifu ili kuweza kupata fursa za kiuchumi.
Wanufaika wa pikipiki hizo wameahidi kuzitunza lakini pia kushukuru wakieleza kuwa zitaweza kuwaongezea kipato chao cha kila siku kwani hazina masharti yoyote magumu.

