Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu na Wananchi wa Mkoa wa Kusini katika Futari ya pamoja aliyowaandalia .


Hafla hiyo ya Futari imefanyika katika Viwanja vya Nje vya Ukumbi wa Dkt. Ali Muhammed Shein, ambapo Dkt,.Mwinyi amewashukuru Viongozi Waumini wa Dini ya Kiislamu na Wananchi waliohudhuria Futari hiyo yenye lengo la kuwaunganisha Wananchi wa makundi mbalimbali.
Rais Dķt.Mwinyi amehitimisha utaratibu wake wa kufutari na Wananchi katika Mikoa yote Mitano ya Zanzibar ,utaratibu anaouendeleza kila Mwezi Mtukufu wa Ramadhan .
Akitoa salamu za Mkoa wa Kusini kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo ,Mkuu wa Wilaya ya Kati Ndg.Rajab Ali Rajab, amemuhakikishia Dkt, Mwinyi kuwa Wananchi wa Mkoa huo wanaendelea kumuunga mkono katika juhudi zake za kuleta maendeleo na kumshukuru kwa kuwaandalia futari hiyo.
Wakati huo huo Rais Dkt.Mwinyi amekabidhi sadaka ya Futari kwa Jumuiya ya Watu wasioona zilizotolewa na Jumuiya ya Zanzibar International Development Organization ZIDO.


