RAIS SAMIA AMEMUASILI MTOTO ALIYETELEKEZWA TABORA

RAIS DKT.SAMIA
English

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuasili Mtoto mchanga wa kike aliyekuwa ametupwa na kutelekezwa huko Wilayani Nzega Mkoani Tabora.

Shughuli ya kumuasili Mtoto huyo imefanyika leo Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Alizaliwa, akatupwa akiwa hana Jina. lakini sasa, Anaitwa Grace Samia Suluhu. ni mtoto aliyezaliwa na Mwanamke, na huenda Mwanamke huyo alibeba Mimba kwa miezi tisa, lakini akaishia kumtelekeza malaika huyo ambaye Tarehe 17 Januari, 2026 aliokotwa eneo jirani na nyumba ya Wageni ya Kasulu, Nzega Mjini.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitapwaki Tukai anasema baada ya kupokea taarifa hizo, alishirikiana na Jeshi la Polisi kumchukua Grace Samia Suluhu na kumpeleka Hospitalini kwa uchunguzi na uangalizi, huku juhudi za kumtafuta Mama yake zikiendelea bila mafanikio.

Rais Dkt. Samia amemkaribisha Mtoto Grace Samia Suluhu katika Familia yake na ameahidi kumpatia malezi, ulinzi na huduma zote muhimu ili akue katika mazingira salama na yenye upendo.

Rais Samia akatoa neno lake kama Mama akisema wanawatupa Watoto hawajui wanalolifanya. Amesema kuliko kumtupa Mtoto ni afadhali akamkabidhi kwenye Mamlaka za kisheria au Kituo cha kulelea Watoto.

Rais samia anasema kila Mtoto aliyezaliwa ni hazina, na hatuijui kesho yake. Ama kwa hakika, kazi na utu.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.