DKT. MWINYI ASHIRIKI MAZISHI YA MAMA WA KAMANDA DAIMA

MAZISHI BUMBWINI
English

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Viongozi mbalimbali wa Serikali katika Maziko ya Bibi Sichana Is-haka Daima Mama Mzazi wa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKU) Kanali Makame Abdalla Daima.

Marehemu Sichana Daima Amefariki Jana wakati akitibiwa katika Hospitali ya Mkoa Lumumba. Awali Dkt. Mwinyi alishiriki Sala ya Maiti katika Msikiti wa Bumbwini Misufini. 

Baadae Mwili wa Bi Sichana ukafikishwa Kijiji cha Bumbini Hasara Roho kwa ajili ya Maziko.

Familia ya Marehemu Bi Sichana ikatoa shukrani kwa waliohudhuria Mazishi hayo.

Maziko hayo yamehudhuriwa na Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Wanafamilia na Wananchi mbalimbali.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema Peponi Amiin.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.