TUME YA UTANGAZAJI KUPATIWA MAFUNZO YA KUZUIA PICHA ZILIZO KINYUME NA MAADILI

TUME YA UTANGAZAJI ZANZIBAR

Tume ya Utangazaji Zanzibar imesema imeandaa Mafunzo ya kuwapatia Watumishi wa Tume hiyo kutoka Mamlaka ya mawasiliano TanzaniaTCRA ili kuwapatia uwezo wa kuzuia Picha zilizo kinyume na maadili kusambazwa katika Mitandao

Akizumgumza na ZBC Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Bw Suleiman Abdulla Salim   amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza na kuondosha Mmomonyoko wa Maadili Nchini.

Amesema Mitandao ya Kijamimi imekuwa ikiwaathiri Watoto kwa kiasi kibwa na kupelekea kuacha kushughulikia Masomo yao, hivyo Mafunzo hayo yatasaidia kudhibiti Picha zisizo na Maadili kutumwa katika Mitandao ya Kijamii na kuwafikia Watoto.

Awali Wazazi na Walezi wamesema Mitandao ya Kijamii imekuwa ni chanzo kikubwa cha Mmongonyoko wa maadili kwa Watoto walio chini ya umri wa Miaka 18  hivyo, wameihimiza Jamii kusimamia Malezi ya Watoto vizuri kwa kuwazuia kutumia Simu wakiwa na umri mdogo

Naye Mkufunzi wa Saikolojia kutoka Chuo cha Abrahaman Alsumait Bw Khamis Juma Khalfan amesema kuna athari nyingi zinazowapata Watoto kwa kutumia Simu wakiwa na umri mdogo ikiwemo Msongo wa mawazo pamoja na Vishawishi vya mambo maovu

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.