MHE.HEMED AZITAKA TAASISI ZA SERIKALI KUFANYA KAZI KWA UADILIFU

MAKAMO WA PILI WA RAIS

   Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdullah ameigaiza Wizara ya Kazi, Uchumi, na Uwekezaji kushirikiana na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi  kuhakikisha Wananchi wanapata Mikopo bila ya  kupewa usumbufu   wakati wanapoiomba.

   Akiakhirisha Mkutano wa Kumi na Tano wa Baraza la Kumi la Wawakilishi   la Bajeti huko  Chukwani  amesema   baadhi ya Wanaanchi wanapata usumbufu  kwa muda mrefu na Hatimae kukosa kabisa   Mikopo hiyo licha ya kuwa  Wanania ya kujiajiri  Wenyewe kwa Kazi za Ujasiri Amali  na kuuagiza Uongozi wa  ZAWA  na ZECO  kuhakikisha  Wanaongeza juhudi ya kusimamaia vyema  upatikanaji wa Huduma ya Maji  pamoja kuwapatia  Wateja wao Nishati Umeme kwa  Wakati.

   Aidha amewataka Madakati na Wauguzi   kutoa huduma bora kwa  maslahi  ya Wizara  na  Wananchi   huku akisisitiza Kampuni za Binafsi   katika Hospitali za  Serikali    kuhakikisha wanatoa huduma bora  ili lengo la Serikali liweze kufikiwa.

   Kuhusu Wazabuni wanaochelewa kukamilisha Miradi wanayopewa na Serikali kwa wakati kwa kuzingatia  Mikataba wanayokubaliana na Serikali Mh.Hemed ameagiza  Mamlaka ya kuzuia Rushuwa na Uhujumu Uchumi  Zanzibar ZAECA kufuatiliwa kwa  karibu kwa kuchukuwa hatua  za kisheria. 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.