Akiakhirisha Mkutano wa Kumi na Tano wa Baraza la Kumi la Wawakilishi la Bajeti huko Chukwani amesema baadhi ya Wanaanchi wanapata usumbufu kwa muda mrefu na Hatimae kukosa kabisa Mikopo hiyo licha ya kuwa Wanania ya kujiajiri Wenyewe kwa Kazi za Ujasiri Amali na kuuagiza Uongozi wa ZAWA na ZECO kuhakikisha Wanaongeza juhudi ya kusimamaia vyema upatikanaji wa Huduma ya Maji pamoja kuwapatia Wateja wao Nishati Umeme kwa Wakati.
Aidha amewataka Madakati na Wauguzi kutoa huduma bora kwa maslahi ya Wizara na Wananchi huku akisisitiza Kampuni za Binafsi katika Hospitali za Serikali kuhakikisha wanatoa huduma bora ili lengo la Serikali liweze kufikiwa.
Kuhusu Wazabuni wanaochelewa kukamilisha Miradi wanayopewa na Serikali kwa wakati kwa kuzingatia Mikataba wanayokubaliana na Serikali Mh.Hemed ameagiza Mamlaka ya kuzuia Rushuwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar ZAECA kufuatiliwa kwa karibu kwa kuchukuwa hatua za kisheria.