Nairat Abdallah Ali ndie Mkurugenzi mpya wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA Zanzibar
Nairat anachukuwa nafasi hiyo kutoka kwa Dkt. Mzuri Issa aliyehudumu katika nafasi hiyo kwa Kipindi cha Miaka 19

Akizungumza katika Hafla ya kumkaribisha Mkurugenzi Nairat amesema amepokea dhamana hiyo kwa kuamini kuwa Uongozi si maneno bali ni vitendo hivyo ataendelea kuisaidia Jamii dhidi ya sheria zisizokuwa na maslahi na Jamii
Mkurugenzi Mstaafu Dkt.Mzuri Issa Amesema anajivunia hatua walofikia sasa kupitia Chama hicho hasa ongezeko la Viongozi Wanawake katika Ngazi za maamuzi, unyanyasaji uliokuwa unawakumba Wanawake kiuchumi na vitendo vya ukatili lakini bado nguvu nahitajika katika kuiweka huru Jamii dhidi ya vitendo hivyo
Akizungumza kwa niaba ya Waandishi wa Habari Khatib Suleiman Gurecha na Huwayda Nassor wamesema kupitia TAMWA Waandishi wa Habari wamejengewa uwezo katika kuandika Makala, Uchambuzi na Habari na kuahidi kuendelea kufanya kazi na TAMWA kwa ajili ya Jamii
Akisoma Risala kwa niaba ya Wafanyakazi Zaina Abdallah Mzee amemtaja Dkt.Mzuri kuwa aliweka msisitizo katika haki na usawa kwa kila mmoja na kuwajenga kifikra na kitaaluma huku akisisitiza msimamo katika kutoa huduma bila ya kujali cheo chake
Dkt.Mzuri Issa Ali alianza utekelezaji wa kazi za Miradi na TAMWA Mwaka 2002 kwa utetezi wa masuala mbalimbali ya Wanawake dhidi ya ukatili wa kijinsia hadi Mwaka 2007 ilipo sajiliwa rasmi TAMWA Zanzibar.
