Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe Mudrik Ramadhan Soraga ameungana na Wananchi katika Dua ya kumuombea aliyekuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa chama cha Afro Shirazi Marehemu Sheikh Thabit Kombo huko Chukwani .
Akizungumza mara baada ya Dua hiyo Waziri Soraga amesema Serikali inathamini mchango uliotolewa na Kiongozi huyo katika harakati za Mapinduzi ya Zanzibar na kipindi chote cha Uongozi wake
Ameeleza kuwa Marehemu Sheikh Thabit Kombo alikuwa Mzalendo na Mwenye kuipenda Nchi yake na kuaminiwa na Viongozi wake katika kufanya kazi nae.
Akitoa Shukrani kwa Niaba ya Familia Mjukuu wa Sheikh Thabit Kombo Bwana Muhsini Muhidini Ali ameushukuru Uongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendeleza utaratibu huo wa kuwaombea Dua Viongozi walio tangulia mbele ya haki .
SMZ INATHAMINI MCHANGO WA MAREHEMU THABIT KOMBO
stories
standard