SMZ INATHAMINI MCHANGO WA MAREHEMU THABIT KOMBO

DUA YA MAREHEMU THABIT KOMBO

Waziri wa  Utalii na Mambo ya Kale  Mhe Mudrik Ramadhan Soraga  ameungana na Wananchi katika  Dua ya kumuombea aliyekuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa chama cha Afro  Shirazi Marehemu Sheikh Thabit Kombo  huko Chukwani .

Akizungumza mara baada ya Dua hiyo Waziri Soraga amesema  Serikali inathamini mchango uliotolewa na Kiongozi huyo katika harakati za Mapinduzi ya Zanzibar na kipindi chote cha Uongozi wake 

Ameeleza kuwa Marehemu Sheikh Thabit Kombo alikuwa Mzalendo na Mwenye kuipenda Nchi yake na kuaminiwa na Viongozi wake katika kufanya kazi nae.

Akitoa Shukrani kwa Niaba ya Familia Mjukuu wa Sheikh Thabit Kombo Bwana Muhsini Muhidini Ali ameushukuru Uongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendeleza utaratibu huo wa kuwaombea Dua Viongozi walio tangulia mbele ya haki  .

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.