BODI MPYA YA PBZ YAZINDULIWA

UZINDUZI BODI PBZ

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Dk. Saada Mkuya Salum amewataka Watendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (Pbz) kuipa ushirikiano Bodi mpya ili waweze kuyapeleka mbele zaidi mafanikio ya Benki hiyo.

    Akizindua Bodi mpya ya Pbz  Dkt.Saada amesema mafanikio yaliyopatikana ni makubwa ukilinganisha na walipotoka ambapo bado kuna fursa katika Soko hivyo anaamini ushirikiano huo utawawezesha kufika lengo la Serikali.  

    Dkt. Saada amefahamisha kuwa mafanikio makubwa ya Serikali yanatokana na mchango wa Benki ya Watu wa Zanzibar hivyo juhudi zaidi zinahitajika ili kupeleka mbele maendeleo ya Benki hiyo na Taifa kwa ujumla. 

    Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Ndg.Joseph Abdalla Meza amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kumuamini na kuahidi kuyafanyia kazi yote waliyoelekezwa  kwa  kufuata sheria zilizopo ili kufikia lengo la kuanzishwa kwa Benki hiyo.

 

 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.