MEGAWATI 49.5 ZA UMEME KWA NGUVU YA MAJI KUONDOA TATIZO LA UMEME

Makubaliano  Biteko

    Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini Makubaliano ya Mkataba na Kampuni ya Dongfang Electric International Corporation ya Nchini China Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Kituo cha  uzalishaji Umeme kwa nguvu ya Maji katika Mto Malagarasi Mkoani Kigoma huku  ikiahidi kumaliza  tatizo la kukosekana kwa  Umeme Nchini.

   Akizungumza mara baada ya kushuhudia kusainiwa kwa Mkataba huo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Doto Biteko amesisitizia usimamizi wa Mradi huo.

   Aidha Dkt.Biteko amemtaka Mkandarasi  kukamulisha mradi huo kwa wakati ili kutimiza kiu ya wana kigoma ya kupata umeme wa uhakika.

    Akizungumza kwa niaba ya Wabunge wa Mkoa wa Kigoma Waziri wa  Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na wenye Ulemavu,Prof.Joyce Ndalichako, Ameishukuru Serikali kwa Mradi wa uzalishaji Umeme Mkoani Kigoma ambao  utatoa fursa ya Ajira kwa Vijana na kuahidi kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa Mradi huo.

    Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)  Mhandisi Gissima Nyamohanga Amesema kuwa Mradi huo unatekelezwa kwa Miezi 42.

 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.