Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini Makubaliano ya Mkataba na Kampuni ya Dongfang Electric International Corporation ya Nchini China Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Kituo cha uzalishaji Umeme kwa nguvu ya Maji katika Mto Malagarasi Mkoani Kigoma huku ikiahidi kumaliza tatizo la kukosekana kwa Umeme Nchini.
Akizungumza mara baada ya kushuhudia kusainiwa kwa Mkataba huo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Doto Biteko amesisitizia usimamizi wa Mradi huo.
Aidha Dkt.Biteko amemtaka Mkandarasi kukamulisha mradi huo kwa wakati ili kutimiza kiu ya wana kigoma ya kupata umeme wa uhakika.
Akizungumza kwa niaba ya Wabunge wa Mkoa wa Kigoma Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na wenye Ulemavu,Prof.Joyce Ndalichako, Ameishukuru Serikali kwa Mradi wa uzalishaji Umeme Mkoani Kigoma ambao utatoa fursa ya Ajira kwa Vijana na kuahidi kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa Mradi huo.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Mhandisi Gissima Nyamohanga Amesema kuwa Mradi huo unatekelezwa kwa Miezi 42.