WANANCHI WAOMBA KASI YA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA IONGEZEKE
Wananchi wa Kijiji cha Kaole Ufundi ,Bagamoyo Mkoani Pwani wameiomba Serikali kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya Dawa za kulevya ili kukomesha biashara hiyo katika Jamii.
Wananchi hao wametoa kauli hiyo wakati Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini DCEA ikikamata virobo 18 vyenye vifurushi 1062 vya dawa za kulevya aina ya Mirungi, Boti ya Mwendokasi pamoja na watuhumiwa Wanne waliokuwa wanasafiri na chombo hicho katika ufukwe wa Magambani Kaole Ufundi, Bagamoyo Mkoa Pwani.
