THTU YAPENDEKEZA MAGEUZI YA MFUMO WA KODI KUONGEZA MAPATO YA NDANI
Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU) kimeishauri Serikali kufanya mageuzi ya kina katika mfumo wa kodi ili kuongeza mapato ya ndani bila kuongeza mzigo kwa wafanyakazi.
Pendekezo hilo limo katika andiko maalum la ushauri kuhusu kodi na uchumi lililowasilishwa serikalini, likilenga kuboresha ukusanyaji wa mapato na kukuza uchumi wa taifa kwa njia jumuishi.
