MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA IMEWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI KIPINDI HIKI CHA MVUA
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Ofisi ya Zanzibar Masoud Makame Faki ametoa tahadhari hiyo alipozungumza na ZBC katika Viwanja vya maonesho ya biashara Nyamanzi Wilaya ya Magharib B.
Amesema Mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa zinaambatana na Upepo mkali pamoja na Radi hivyo ni vyema kuchukua tahadhari kwa Wavuvi na Familia zinazoishi maeneo hatarishi.