MTAALA WA MICHEZO KUIBUA VIPAJI TUMBATU
Kurejeshwa Mtaala wa Masomo ya Michezo kwa Wanafunzi kutasaidia kuibua na kuimarisha vipaji vya Michezo mbali mbali katika jamii.
Wakizungumza katika Ziara ya Waandishi wa Habari katika Kisiwa cha Tumbatu,
Mratibu wa Michezo na utamaduni Wilaya Kaskazini 'A' Khamis Hija Mohammed na
Sheha wa Shehia ya Uvivini, Ngwali Sheha Haji, wamesema hapo awali kulikuwa na Wanafunzi waliojishughulisha na Michezo na kufanikiwa kushiriki vyema mashindano mbali mbali.