HISPANIA YANYAKUA UBINGWA WA EURO 2024
Hispania imenyakua ubingwa katika michuano ya EURO 2024 baada ya kuichapa England mabao 2 - 1.
Mabao ya Hispania yamefungwa na Nico Williams 47' na Mikel Oyarzabal 86' huku goli pekee la England likifungwa na Cole Palmer 73'.
Fainali hiyo imepigwa katika dimba la Olympiastadion huko Berlin, Ujerumani.
Hii ni mara ya nne kwa Hispania kunyakua ubingwa katika michuano hiyo na EURO na England yenyewe haijawahi kuchukua ubingwa hata mara moja katika michuano hiyo.